Harmonize amefanikiwa kutengeneza CV mpya ya maisha yake ya muziki katika mtandao wa Youtube kupitia wimbo wake wa ‘Bado’ aliomshirikisha Diamond.
Wimbo huo ambao umewekwa kwenye mtandao huo mwezi Februari mwaka jana umefanikiwa kutazamwa mara milioni 10.3 kwenye mtandao wa YouTube na umekuwa wimbo wa kwanza kwa msanii huyo kutazamwa mara nyingi zaidi. Lakini pia Bado umeingia kwenye orodha ya video chache za wasanii wa muziki nchini kufikisha idadi hiyo ya kutazamwa.
Baada ya kujitengenezea rekodi hiyo, Harmonize ameandika waraka kupitia mtandao wa Instagram unaosomeka:
Nitangulize shukrani za dhati kwenu ndugu zangu mnao endeleu ku support sanaa yangu sasa hivi wimbo huu #Bado umeingia katika histor na kuwa nembo ya nchi yetu Tanzania kwa kufikisha idadi ya watazamaji million 10 ni Video chache sana Tanzania zilizo wahi fikisha idadi hii ya watazamaji nyimbo ninazo zikumbuka kuwa zimefanikiwa kuwa nembo ya taifa letu kwa kufikisha idadi ya watazamaji wengi( 1) #Nana Diamond platnumz milion 20 (2) Number one Diamond platnumz million 19 (3) Nitampatawapi Diamond platnumz million 11 (4 ) #Salome Diamond platnumz million 11 inayofwata #Bado Harmonize ft Diamond platnumz million 10 kikubwa na washukuru na nawaahidi kuto waangusha naombeni mzidi ni supportnitajie na nyingine niliyo isahau hapa ambayo imefikisha million 10 tafadhali……..!!!!
0 comments:
Post a Comment