Sunday, January 15, 2017

Multichoice imefurahishwa sana na matokeo hayo na kwamba wataendelea kumuunga mkono na kumdhamini Simbu kwa mujibu wa makubaliano yao, ili kuhakikisha anaendelea kufanya vyema na kuliletea Taifa sifa kubwa.“Tulichukua jukumu la kumdhamini simbu katika mazoezi na maandalizi yake kwa kipindi cha mwaka mzima, kwani tunafahamu fika kuwa mazoezi na maandalizi ndiyo siri kubwa ya mafanikio katika mchezo wowote. dhamira yetu kubwa ni kuinua vipaji na kulirejesha taifa letu kwenye ramani ya dunia katika ulingo wa michezo na burudan  
Mtanzanian aibuka mshindi Mumbai Marathon!
• Awatimulia vumbi Wakenya, Waethiopia.
• Asema ni Ushindi wa Watanzania
Mtazania Alphonce Simbu, ameibuka mshindi wa mashindano ya Mumbai Marathon ya mwaka huu huku akimtimulia vumbi Mkenya Joshua Kipkorir katika kundi la wakimbiaji wa nje. Ttanzania huyo aliongoza huku akifuatiwa na Wakenya 7 and Waethiopia 2 katika 10 bora.
Mashindano hayo yajulikanayo kama Standard Chartered Mumbai Marathon yanafanyika kila Jumapili ya tatu ya mwezi Januari katika jiji la Mumbai nchini India na ni mbio zinazoaminika kuwa kubwa kabisa barani Asia kwa idadi ya washiriki wanaombaliza.
Simbu, ambaye anadhaminiwa na kampuni ya Multichoice Tanzania, aliibuka mshindi kwa kutumia muda wa 2:09:28 muda ambao ni mzuri sana kwa mbio za aina hiyo.
Akizungumzia ushindi wake, Simbu amesema kuwa anaamini ushindi huo umesababishwa na maandalizi aliyoyafanya na kwamba udhamini wa kampuni ya Multichoice Tanzania umemsaidia sana kwani imekuwa rahisi yeye kutumia muda mwingi zaidi kwenye mazoezi na maandalizi.
Amesema anauchukulia ushindi huo kama changamoto kwa mashindano mengine makubwa na kwamba huo ni mwanzo tu. Amesisitiza kuwa ushindi huo siyo wake peke yake au Multichoice , bali ni ushindi wa Taifa zima la Tanzania.

0 comments:

Post a Comment