Mtoto
wa miaka 10 kutoka Indonesia, ambaye ametajwa kuwa mtoto aliyenenepa
zaidi duniani alianza kupewa chakula cha kupunguza uzito Arya Permana
ameorodheshwa kuwa na unene usio wa kawaida kwa kuwa alikuwa na uzani wa
kilo 188.
Mtoto huyu hatimaye ameweza kurudi shuleni baada ya
kupunguza uzito wa kutosha wa kumwezesha yeye kutembea kwani siku zote
alikuwa akillala na hakuweza kutembea na kusababisha yeye kukatisha
masomo.
Mtoto huyu unaambiwa amekuwa akila milo mitano kwa siku
lakini baada ya ushauri wa kufanya diet na mazoezi makali Arya ameanza
kupunguza uzito ndani ya wiki chache sasa anaweza kukaa lakini pia
kutembea kwenda shule na kucheza na wenzake darasani
0 comments:
Post a Comment