Mwanaharakati
nchini India Irom Sharmila anakamilisha mgomo wake leo wa kukataa kula
chakula kwa miaka 16 ikiwa ni adhima yake ya kupinga sheria tata ya
ukatili ambapo maofisa wa jeshi wamepewa mamlaka ikiwemo kupiga risasi
na kuuwa raia nchini humo, jambo ambalo ameliita ni unyanyasaji na
ukiukwaji wa haki za binadamu.
Mwanaharakati
huyo ameachiliwa huru na anatarajia kuanza kula hii leo baada ya
Mahakama katika Jimbo la Manipur lililopo Kaskazini Mashariki mwa nchi
hiyo.
Lakini
mwezi uliopita aliiambia mahakama kwamba anataka kukatiza mgomo wake na
kuanza kampeni yake kama mgombea huru katika uchaguzi ujao wa wabunge .
Mpiga picha Ian Thomas Jansen-Lonnquist alifuatilia kwa karibu safari yake katika miaka michache iliyopita.
Ameishi
kipindi kirefu cha miaka 16 chini ya uangalizi wa mahakama katika
Hospitali ya Mji Mkuu wa Jimbo la Manipur, Imphal, ambako alilazimishwa
kunywa mchanganyiko wa madawa na maziwa ya unga ya watoto wachanga
Bi
Sharmila aliachiliwa huru mwezi Agosti 2014 baada ya mahakama kukataa
shitaka kwamba “anajaribu kukujiua “. Lakini alikamatwa tena siku mbili
baadae baada ya kukataa kumaliza mgomo wake.
Bi Sharmila alikuwa akihudhuria Mahakama Kuu ya Manipur kila baada ya wiki mbili kurejelea msimamo wake mgomo.
Mwanaharakati
huyo alivivutia vyombo vya habari vya ndani ya nchi na vya kimataifa
katika miaka ya hivi karibuni. Bi Sharmila alikua na ufuasi wa wanawake
na makundi yanayopigania haki za kijamii katika jimboni.
0 comments:
Post a Comment