Unapokuta
mwanamke au mwanaume anamlaumu mume au mke wake kwa kitendo chake cha
kukaa na kuzungumza na mtu wa jinsia nyingine mara kwa mara utasemaje,
je utasema ni wivu uliopitiliza ?.Inawezekana
ikawa ni wivu, lakini kwa upande wa pili, huenda haitokani na wivu,
bali ukweli kwamba, watu wawili wa jinsia mbili wanapozoeana katika
kuzungumza, hatimaye uwezekano wa kukutana kimwili hujitokeza.
Kwa
kupitiwa au kujisahau, wanawake wengi huwa wanawapa nafasi marafiki au
shoga zao kuwa karibu na waume zao kwa kuzungumza, wakiamini kwamba,
kuzungumza tu, hakuwezi kuwa na madhara. Huku ni kujidanganya kwa kiasi
kikubwa.
Kwa
kadiri watu wa jinsia mbili wanavyozoeana katika kuzungumza na hasa
wanapoanza kuzungumzia mambo yao ya ndani, ndivyo ambavyo mipaka huvukwa
na kujikuta wakihusiana kimwili.
Pale
mpenzi kuwa karibu mara nyingi na mtu mwingine wa jinsia tofauti kwa
maelezo kwamba, ‘ni rafiki tu,’ ujue tatizo liko karibu kuanza kama
halijaanza. Kuwa karibu sana kwa mazungumzo mara kwa mara na mtu wa
jinsia nyingine, ni aina ya uzinzi pia, kutegemea tu aina ya mazungumzo.
Labda
nijaribu tu kuwasaidia wale ambao wako kwenye uhusiano tayari.
Wanapohisi dalili fulani, kuhusiana na rafiki zao wa jinsia tofauti,
wanapaswa kujua kwamba, hivi karibuni, urafiki huo utaisha na watakuwa
wapenzi. Kama hawataki kuharibu uhusiano waliomo, wanapohisi dalili hizi
wanapaswa kujitoa.
Kama
mtu ana rafiki wa jinsia tofauti, ambaye siku zote amekuwa akijiambia
ni marafiki tu, anapojikuta ameanza kumwotea ndoto za mchana kama za
Alinacha, ni hatari. Kumwotea ndoto za mchana rafiki wa jinsia tofauti
si dalili nzuri hata kidogo na haiashirii jambo jema huko mbeleni.
Kama
mwanaume ana rafiki wa jinsia tofauti na anapokuwa na jambo au mambo ya
kutaka mtu mwingine ayasikie ili ahisi nafuu, anayaweka kwa ajili ya
rafiki huyo, badala ya kumwambia mkewe, urafiki huo utageuka balaa sasa
hivi.
Kuna
wanaume ambao hata kama ametaka kugongwa na gari, hatazungumza jambo
hilo na mkewe, bali atangoja akikutana na huyo rafiki yake wa jinsia
tofauti ndiyo amweleze. Hata kama mwanaume huyu hajashiriki tendo la
kujamiiana na rafiki huyo, uwezekano ni kwamba, bado kitambo kidogo
watashiriki.
Mwanaume
anapoona na kuamini kwamba, rafiki yake wa jinsia nyingine anamwelewa
vizuri zaidi kuliko mkewe, ni wazi kabisa kwamba, hiyo ni hatari, kwani
ni safari ya moja kwa moja kuelekea kushirikiana kimwili.
Kama
imefikia mahali ambapo mume anashiriki kujadili siri za mke wake na
rafiki wa jinsia nyingine ni dalili mbaya kwamba, watu hao kama
hawajaanza kushirikiana kimwili, wataanza muda mfupi ujao.
Mwanaume
kuanza kumnunulia rafiki wa jinsia nyingine nguo za ndani, pafyumu,
mapambo na vitu vya aina hiyo. Jambo hilo ni ishara kwamba, ile, ‘ni
rafiki yangu tu,’ itafutika sasa hivi na watu hao watakuwa wapenzi.
Mwanaume........Kama
uko kwenye urafiki ambao una dalili hizo, ni vema kuanza kukagua
mwenendo wako na huyo rafiki yako. Kama hutaki kutoka nje ya ndoa yako,
inabidi au ujitoe kwenye urafiki huo, au uache kufanya hayo mambo
niliyoyaeleza.
Namalizia
kwa kuwaambia wanawake kwamba, huna haja ya kumwacha huru shoga yako na
mumeo kwa kudhani ni vigumu kwa watu hao kukusaliti. Wakianza kushiriki
mazungumzo ya kihisia haraka sana wataingia mahali ambapo watataka
kushirikiana kimwili.
Hata
wao katika hatua za awali watakuwa hawana lengo la kushiriki tendo la
kujamiiana, lakini mazungumzo yao, hatimaye yatawafanya waungane kihisia
na kitakachofuata kitakuwa ni maumivu kwako.
Weka
mipaka ya makusudi, onesha kutoridhishwa na mume au mpenzi wako ama
shoga yako unapoona mmoja au wote wanajisahau na kuanza kuwa karibu sana
kimazungumzo.
Suala
la ‘shogako leo alipita ofisini kwangu,’ kutoka kwa mume au mpenzi
wako, usilikubali kirahisi. Suala la ‘nasikia shemeji anasafiri, naomba
anipe lifti, na mie naenda Morogoro,’ usikubali kirahisi. Bora uambiwe
una wivu kuliko kuja kupoteza……
Source:Jamii Forums
You might also like:
0 comments:
Post a Comment