Mwanamume
mmoja nchini India inasemekana hakuwa na uwezo kifedha ili kuweza
kusafirisha maiti ya mkewe kwa kutumia gari ya kubebea wagonjwa hadi
kijijini kwao na hivyo ikambidi kuibeba maiti ya mkewe kwa umbali wa
zaidi ya kilomita 12, kutoka hospitali aliyofariki, kwani ilishindwa
kumsafirisha kwa gari la kuwabebea wagonjwa hadi kijiji mwake.
Mke
wa Dana Mjhi, Amang, mwenye umri wa 42, alilazwa hospitali ya Ulaya,
mji wa Bhawanipatna jimbo la Orissa. siku ya Jumanne na alifariki dunia
siku inayofata kwani alikua akiugua maradhi ya kifua kikuu. katika Bwana
Mahji alisema kijiji chake kilikuwa umbali wa kilomita 60 na hakuwa na
uwezo wa kulipa gharama ya usafiri wa gari la kuwabebea wagonjwa.
Bwana
Mahji, ilimbidi achukue maiti hiyo kwani kwa madai yake wahuduhu
walimsihi kufanya hivyo, na alipowaomba wamsadie gari ya kubebea maiti
hakuweza kupata ndipo uamuzi wa kumbeba mkewe begani na kuanza safari
kuelekea kijijini Melghar kufuata mila na tamanduni za mwisho huku
akiungana na mwanawe mwenye umri wa miaka 12
Alitembea
kwa takriban kilomita 12, ndipo watu walipoingilia kati na wakaamua
kumsaidia gari la kubebea wagonjwa mpaka wakamfikisha hadi mwisho wa
safari yake ambako shughuli ya kuchoma mwili wa mkewe ilifanyika siku ya
Jumatano usiku.
0 comments:
Post a Comment