Bila kufahamika chanzo ni nini taarifa zisizo rasmi zimetrend katika mitandao ya kijamii zikidai kuwa mkongwe wa filamu hapa nchini King Majuto amefariki dunia kwa ajali ya gari.
Soudy Brown akaona sio kesi, akaamua kumvutia waya Mzee Majuto na kujua undani wa taarifa hizo. King Majuto amefunguka kuwa sio mara ya kwanza kwa yeye kuzushiwa kifo, ila tu anashangaa ni kwanini hali hiyo inajirudia mara kwa mara kwa upande wake.
Play hii video hapa chini kumsikiliza Soudy Brown akipiga story na Mzee Majuto kuhusiana na tetesi hizo.
0 comments:
Post a Comment