Friday, January 6, 2017

Tukiwa bado tunaendelea kuenjoy ngoma ya “Sijiwezi” kutoka kwa Nay wa mitego, inaonekana kama Nay amefunguka kuhusu yeye kutokana na mambo ambayo bado yapo vichwani mwa mashabiki kuhusu ishu yake na Mr T Touch.

Baada ya kutupatia posti ya kutuonjesha mashabiki zake tukae tayari kwa ujio wa kitu kipya kutoka kwake kwenye kurasa yake ya Instagram kwa kusema kwamba ‘MrPretender
😂
 Anza ku Subscribe kwenye YouTube Chanel Yangu #MrNay Nina jambo Kubwa kwa ajili yako soon. Go and Subscribe to my YouTube Chanel #MrNay i got something big for you. Soon.’Nay alitumia kurasa yake tena kuongelea kuhusiana na yeye alipotoka mpaka kufikia hapa huku akiongeza kuwa hana Roho mbaya ndio maana Mungu anampa zaidi.

Ujumbe huo wa Nay umewafanya mashabiki kuunganisha na ishu ambayo ilitokea jana ya Mr T Touch wakati alipokuwa Clouds Fm kwenye kipindi cha XXL kufunguka mengi kuhusu Nay wa mitego.
Inaweza kuwa ni jambo gumu la hawa jamaa kurudi pamoja na kutengeneza vyombo kama zamani, ila unahisi kipi kifanyike kwa washikaji zetu hawa, nini liwe suluhisho baina yao?.

0 comments:

Post a Comment