Wednesday, January 18, 2017

Baada ya kuingia kwenye listi ya mastaa ambao waliuanza mwaka vibaya kwa kushindwa kuimba nyimbo zake vizuri wakati wa show yake ya kufungua mwaka mpya wa 2017, Nick Cannon amejitokeza kumtetea Mariah.

Kama utakumbuka siku ya kuukaribisha mwaka mpya Mariah Carey aliingia kwenye majanga mazito baada ya kushindwa kuimba vizuri kutokana na kutosikia mdundo wa muziki uliokuwa na sauti katika earphones zake alizokuwa amevaa na kumfanya kumpelekea kuanza kuongea badala ya kuimba.
Jambo hilo lilimfanya Mariah Carey kuongea mengi baada ya ishu hiyo kuwa kama alifanyiwa makusudi kwenye tamasha hilo, sasa Nick Cannon aliamua naye kufunguka juu ya ishu hiyo wakati alipokuwa anahojiwa na “Ellen” kuongelea maswala yake ndipo akafunguka kwa kusema kwamba vyote vile vilikuwa mtego wa kutaka kumdhalilisha Mariah Carey.
You know me, I’m a conspiracy theorist I think the government did that. They set her up. That was a distraction. They just put her out there. I mean, anyone who knows about performing and having in-ears and stuff, things like that can go wrong on live television. I do live television all the time. I screw up on America’s Got Talent all the time. When there’s people in your ears, saying things and stuff, I think she kinda got a little flustered. Alifunguka Nick Canon.

0 comments:

Post a Comment