Thursday, January 12, 2017

Haya sasa mwaka mpya na couple mpya, The Weeknd na mwanadada Selena Gomez mambo kama yameshamiri hivi ya kimahaba.


Kupitia picha zilizopigwa kwa siri na kuachiwa na mtandao wa Tmz, unawaonyesha The Weeknd pamoja na Selena Gomez wakiwa wanaKiss walipokuwa wanatoka kwenye mgahawa wa Giorgio Baldi huko Santa Monica siku ya jumanne.
Ndani ya picha hiyo inamwonyesha Selena akiwa amemkumbatia kabisa The Weeknd huku akimpa busu la shavu.


Kama utakumbuka kipindi cha nyuma Selena Gomez aliwahi kuwa kwenye mahusiano na msanii Justin Bieber na upande wa pili wa The Weeknd naye amewahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na model Bella ambaye taarifa zinasema kwamba wawili hao walishaachana muda mrefu.
Bado hakuna taarifa rasmi kama wawili hawa wapo kwenye mahusiano zaidi ya kuona picha wakiwa pamoja na kupeana Kisses hizo.

0 comments:

Post a Comment