Diamond Platnumz amemchukua kijana wake Ray Vanny kwaajili ya kutumbuiza naye Alhamis hii kwenye tuzo za shirikisho la soka barani Afrika, CAF zitakazotolewa mjini Abuja, Nigeria.
Wawili hao watatumbuiza wimbo wao uliokuwa wa pili kwa ukubwa Afrika mwaka jana (baada ya Pana ya Tekno), Salome.
“GloCafAwards rehearsal na Vanny Bway!!! Tomorrow will be performing your favorite Song #SALOME na @rayvanny #GLOCAFAWARDS,” ameandika Diamond kwenye picha aliyoiweka Instagram.
Ray Vanny akiwa nje ya hoteli waliyofikia mjini Abuja
Naye Ray Vanny ameshare picha kadhaa akiwa kwenye ukumbi zitakapotolewa tuzo hizo akifanya rehearsal na bosi wake. Pia ameshare video akizungumza na mastaa wengine watakaotumbuiza kwenye tuzo hizo akiwemo Yemi Alade na Flavour.
Ray Vanny akiwa na msanii wa Mavin Records, Reekado Banks
Ray Vanny na Diamond wakifanya mazoezi kwaajili ya show yao ya leo kwenye tuzo za CAF
Wasanii wa Afrika Kusini, Muffinz nao watatumbuiza. Pia Dj nguli wa Nigeria, Jimmy Jatt atakuwepo kuburudisha. Tuzo hizo zitaruka live kuanzia saa 12 jioni saa za Afrika Mashariki hadi saa 4 usiku kupitia Supersport Channel 4 (204), SS 9 (209) ana kupitia GOTV.
0 comments:
Post a Comment