Chama cha Mapinduzi nchini Tanzania kimesema kinachofanyika hivi sasa ndani ya chama hicho ni mageuzi na wala siyo mabadiliko ya kawaida, kwa kuwa mageuzi ni zaidi ya mabadiliko, lengo likiwa ni kuwa chama makini cha siasa kwa ajili ya maendeleo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho Humphrey Polepole, amesema katika mageuzi yatakayofanyika hivi sasa ndani ya chama hicho yatagusa maeneo matatu ambayo ni pamoja na eneo la uongozi kwa kuweka viongozi waadilifu, eneo la pili ni mfumo ili chama kiwe na tija, na eneo la tatu ikiwa ni utawala.
0 comments:
Post a Comment