Kumekuwa na maneno ya chini chini tangu tu hitmaker wa ngoma ya Moyo Mashine Benpol alipotangaza kuwa ameachia wimbo mpya ambao kamshirikisha Mnigeria Mr Eazi (Phone).
Maneno ambayo yaliwahusisha maproducer wawili na wakali wa muziki Tiddy Hotter na Sappy kutokana na kile ambacho Sappy anadai kuwa Tiddy Hotter ameiba idea yake kwenye wimbo wa Phone.
Sappy anadai kuwa picha lilianza mwezi December mwaka 2015 ambapo alidondoka pande za 255 Tanzania na msanii wake afahamikae kama Elvix ndipo wakadondoka mjini Mwanza kwenye studio za Tiddy Hotter na kuhitaji kufanya kazi lakini kwa bahati mbaya kazi hiyo haikumalizika kutokana na muda na vitu kama hivyo.
Unaweza kuupata uhondo full kwa kumsikiliza mwenyewe akifunguka juu ya issue hiyo ilivyoenda kwa kuplay hii video hapa chini.
Haikuishia hapo, baada ya kutusomesha mchongo mzima jinsi ilivyokuwa katika utengenezaji wa kazi hiyo. Sappy alitusanua kuwa ni kitu gani ambacho anahitaji kutokana na kitendo hicho cha Tiddy Hotter kuiba idea na kuitumia bila kumjulisha chochote.
Kufuata sheria ndio kitu ambacho Sappy aliamua kufanya na kuiachia sheria ichukue mkondo wake au kama sio hivyo wagawane asilimia katika mapato ya wimbo huo. Bonyeza play kwenye video hii hapa chini kumsikiliza akifunguka juu ya hilo.
XXL ya Clouds Fm haikuona poa kuukamilisha mchezo bila kumtafuta producer Tiddy Hotter na pia kusikia ambacho anacho producer huyo kuhusiana na tuhuma hizo.
Chakushangaza ni kwamba Tiddy Hotter amekanusha vikali tuhuma hizo na kudai kuwa kila kitu amehusika yeye kwenye ngoma hiyo mpya ya Benpol ila tu Sappy ameamua kumchafua.
0 comments:
Post a Comment