Friday, January 27, 2017

RAIS WA GAMBIA ADAMA BARROW AWASILI NCHINI MWAKE, Rais wa Gambi Adama Barrow amewasili nchini humo akitokea nchini Senegal.Kiongozi huyo akiwa chini ya Ulinzi mkali wa vikosi vya ECOWAS, amewasili nchini mwake kwa ndege ya ECOWAS.Atakaa kwa muda nyumbani kwake kabla ya kukaa Ikulu ambayo inafanyiwa uchunguzi wa kiusalama.
Barrow aliapishwa wiki iliyopita Senegal wakati viongozi wa kieneo walipokuwa wakimshawishi kiongozi aliyekuwepo ajiuzulu. Wanadiplomasia wamemtaka Barrow arudi mara moja nyumbani kuepuka pengo la uongozi.
Adama Barrow, akishuka kwenye ndege ya ECOWAS, mjini Banjui. Picha ya Aljazeera
Maelfu kadhaa ya wanajeshi wa mataifa ya Afrika magharibi wanasalia Gambia wakati kukiwa na taarifa kuwa wafuasi waovu wa Jammeh wamo miongoni mwa vikosi vya usalama nchini.
Alipokelewa na umati mkubwa wa wafuasi wake.
Msemaji wa serikali ya Adama Barrow,Halifa Sallah amesema wanajiandaa kufanya sherehe za uapisho na Adama Barrow, kulihutubia taifa.

0 comments:

Post a Comment