Tuesday, January 31, 2017

Kwa mara ya kwanza tangu amuanike katika mitandao ya kijamii mchumba wake anayejulikana kwa jina moja la Remy, mkongwe wa Muziki wa Bongo Fleva, Ambwene Yessaya ‘AY’ aweka wazi alivyompata.

AY adai ilitokana na kumpenda msanii wa Nigeria, Helen Folasede Adu ‘Sade Adu au Sade ambaye anafanana naye kwa asilimia kubwa.
16228575_458617187860497_6501105345266450432_n
AY
AY anayebamba kwa sasa na Ngoma ya More n More aliomshirikisha Nyashinski kutoka Kenya alisema kuwa, Sade ni mwanamuziki aliyemvutia kwa muda mrefu na kumfanya atafute mwanamke anayefanana naye.
“Ni kati ya wanamuziki wachache duniani wanaopendwa sana, anafanya vitu kwa kufikiria na ndiyo maana kazi zake zinadumu  na hata muonekano wake ni mzuri, ni mrembo sana, hazeeki na hana skendo za ajabuajabu kama wengine.
Kingine wanamuziki kama Dr Dre, Mr Chicks, Jay Cole, Jay Z wanamkubali sana. Nakumbuka rapa, Snoop Dogg aliwahi kusema kabisa kuwa, siku akifanya kolabo na Sade basi anastaafu kufanya muziki”. Alisema AY alipozungumza na Over Ze Weekend.
MCHUMBA-WA-AY
Remy & AY
Aliongeza, “Ni kama miaka minne hivi tumefahamiana na Remy, lakini haimaanishi kuwa ilikuwa ni lazima awe na sifa zote za Sade ndiyo awe na AY, sema ninacho shukuru ni kweli ana baadhi ya vitu anafanana naye”.

SADE NI NANI?

Ni mwanamuziki kutoka jamii ya Wayoruba, aliyezaliwa mwaka 1959, Ibadan katika Jimbo la Oyo nchini Nigeria ambaye mama yake ni raia wa Uingereza nafasi ambayo ilimuwezesha kuishi na kupewa uraia wa nchi hiyo.
Sade
Helen Folasede Adu ‘Sade Adu ‘SADE’
Akiwa na Bendi ya Sade amefanikiwa kuachia album kibao ikiwemo Diamond Life (1984), Absolute Beginners (1986), Stronger Than Pride (1988) and Love Deluxe (1992) Lovers Rock (2000), Soldier of Love (2010) na nyingine kibao. Sade pia anatambulika kama Mwanamuziki Bora wa Solo wenye Mafanikio nchini Uingereza.
Sade amewahi kuteuliwa kuwania tuzo 42 tofautitofauti ikiwemo American Black Achievement, American Music, Billboard Music, Brit, Grammy, MOBO, MTV Video Music, NAACP Image, Porin na nyingine kibao.

0 comments:

Post a Comment