Saturday, January 7, 2017

Rapa Nay wa Mitego ambaye hivi sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Siwezi' amefungaka na kuweka wazi sababu ambazo zinafanya vijana wengi kushindwa kufikia malengo yao na kuweka wazi njia za wao kupita ili kufikia mafanikio makubwa katika maisha.

Nay wa Mitego akiongea kwenye kipindi cha Wakilisha cha EATV alisema vijana wengi wanashindwa kufanikiwa kutokana na ukweli kwamba hawajitambui na hawajui wanataka nini huku wengine wakiendekeza sana starehe kuliko hata kipato chao.
"Unajua ukitaka kufanikiwa katika jambo lolote kwanza lazima ujitambue, ujue unataka nini wapi unataka kufika na utafikaje hapo, tatizo vijana wengi siku hizi hawajitambui lakini pia tunakuwa na kampani za watu ambao si watu sahihi yaani naweza kusema kampani ambazo si rafiki na ndoto zako, unakuta una kampani ya watu wanaopenda sana starehe, kuvaa sana pasipokuwa na malengo mwisho wa siku unashindwa kufikia ndoto zako" alisema Nay wa Mitego 
Rapa huyo aliendelea kusisitiza kuwa ili uweze kufanikiwa katika maisha na kuwa na maisha mazuri lazima ujitambue na kupunguza marafiki ambao hawana msaada katika maisha yako, watu ambao wanaweza kukurudisha nyuma na unapaswa kuwa na kampani ya watu ambao wanaweza kukusaidia kufikia malengo yako. 

0 comments:

Post a Comment