Wednesday, January 25, 2017

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amemshukuru Rais Dkt John Magufuli kwa kuleta magari yaendayo kasi jijini Dar es Salaam.
Amesema kwa sasa adha ya usafiri wa umbali mrefu imepungua na umekuwa ni usafiri wa masaa machache ukilinganisha na siku za nyuma.
Ametoa shukrani hizo leo hii jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa magari hayo, eneo la Gerezani, Kariakoo jijini Dar huku akitolea mfano usafiri wa Kimara ulivyokuwa wa tabu na unaotumia masaa mengi.
“Nikupongeze Rais Magufuli na Profesa Makame Mbarawa kwa kuketa magari haya ya mwendokasi. Tunashukuru sana kwa mkoa wetu maana tulikuwa tukisafiri kwa kutumia hata masaa matatu kufika Kimara. Tena tunashukuru rais wetu ameishi sana katika jiji hili alikuwa anatambua adha ya usafiri, lakini kwa sasa hivi tunateleza tu dakika kama 40 unafika nyumbani bila wasiwasi bila foleni kwa kutumia magari haya ya mwendokasi,” amesema Makonda.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kiserikali ambapo baadhi yao ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Angellah Kairuki, Waziri wa fedha na mipango, Philip Mpango,na waziri wa Tamisemi, George Simbachawene. Wengine ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi,na Mstahiki Meya wa Kinondoni, Benjamin Sitta.

0 comments:

Post a Comment