MTUNZI: George Iron Mosenya
SEHEMU YA KWANZA
Aliitazama nchi hii kwa mbali sana, aliyekuwa mkuu wake
alimuonyesha kwa kutumia kidole kimoja. Ilikuwa ina rangi ya bluu hii ndio
ilikuwa nchi kubwa aliyokuwa ameagizwa kumfanyia kazi yake ambayo hakuwa
ameshurutishwa kuifanya bali kwa hiari yake mwenyewe. Baada ya kuelekezwa vyema
katika nchi hii sasa alimuelekeza vi-nchi vingine vidogo vidogo ambavyo
havikuwa na ukubwa wa kutisha.
Majina yake mengi yalikuwa ya kigeni lakini yalieleweka
na kukaa vyema katika kichwa cha kijana huyu aliyekuwa anaelekezwa. Alitikisa
kichwa juu na chini kuashiria kuwa anaelewa somo alilokuwa anapewa.Mkuu wake aliyefahamika kwa jina la Tuntufye Kanyenye ama kwa kifupi Tuntu alitoa tabasamu ambalo kwake lilikuwa bora lakini linatia karaha ukilitazama. Tabasamu hili lilimaanisha kuwa alikuwa na imani kubwa na kijana huyu aliyekuwa anaagizwa katika nchi hii ya bluu na nyingine ndogo ndogo.
“Nakutakia safari njema yenye mafanikio….” Tuntu alimtamkia kijana wake huku akimpapasa kichwa chake katika hali ya kubariki. Baada ya hapo akampulizia marashi fulani katika nguo zake. Halafu akamtwaa na kumnyanyua juu juu tayari kwa kumrusha katika dunia hiyo. Hofu ikaanza kumtawala kijana huyu akawa anatetemeka ujasiri aliokuwanao ukaanza kuyeyuka akawa anatweta kwa hofu lakini tayari alikuwa katika mikono hii mibaya yenye nguvu. Akiwa bado katika uoga mara alirushwa kwa nguvu zote akauacha ule ulimwengu akawa anaelekea katika ulimwengu mwingine. Alikuwa anarusha miguu huku na kule lakini aliishia kuipatia majeraha hewa ambayo ilikuwa katika kila sehemu.
Kwa takribani dakika tano nzima alikuwa hewani na sasa alikuwa anakaribia kutua katika nchi hii ya bluu. Uoga ukamzidi akajikunyata akauziba uso wake kisha akapiga kelele kubwa sana za uoga huku akijaribu kukwepa asitue eneo lile aliloliona kuwa la hatari sana.
Jasho kali lilikuwa linamtoka, alikuwa peke yake chumbani alikuwa amekaa kitako katika kitanda chake cha futi tano kwa sita. Alikuwa anatetemeka. Taa ilikuwa imezimwa akasimama aweze kwenda kuiwasha lakini akajihisi kuwa alikuwa katika kutetemeka, akarudi akaketi tena. Alikuwa ametoka kuota ndoto mbaya sana ambayo hajawahi kuiota kabla. Alijaribu kupikichapikicha macho yake ili aweze kuona kama aliyoyaota yalikuwa ndani ya chumba kile lakini hapakuwa na mfano wa kitu kama hicho pale ndani. Kwa unyonge akarejea kitandani akauchapa usingizi tena.
Palipokucha hakuwa na kumbukumbu tena kama usiku ule alikuwa ameota ndoto mbaya. Aliamka akiwa na amani tele. Alijisikia mwenye nguvu za kustaajabisha!!
Hakujua kama alikuwa ameingia katika utumwa
Utumwa wa bila kujua.
****
Hassan alikuwa anazipitia post za hapa na pale katika mtandao wa
kijamii wa facebook katika namna ambayo hakuwahi kuifanya hapo kabla.
Alizitazama post za mapenzi hasa hasa za wasichana, hakujalisha kama ni warembo
ama la. Hakuwahi kufikiria kuwa siku moja anaweza kuwa kama alivyo.
“Beatrice Cosmas” alilisoma jina hilo na kulirudia mara kwa mara, “Saint Augustine Mwanza” akakisoma na hicho chuo alichokuwa anasoma dada huyu.
“Nipo njiani nakuja Dar yeyote aje kunipokea jamani” hatimaye akaikariri na ile post aliyoweka dada huyu mnene katika picha akiwa na mwanya na macho ya kuvutia.
Hassan aliingia katika inbox ya dada huyu akamkaribisha Dar huku akimwomba ampe nafasi ya kumpokea mara atakapofika. Beatrrice akazuga kujizungusha zungusha na kumwomba Hassan namba yake ya simu na kuahidi kumpa taarifa baada ya kufika. Hassan bila kinyongo alimpatia namba yake ya simu huku akitoa tabasamu.
Hassan aliingia katika shughuli zake huku akiwa ameanza kusahau kama alikuwa na ahadi ya kupokea simu yoyote ile mpya. Ilikuwa kama bahati ya kipekee baada ya kuwa amepokea malipo baada ya mauzo ya mzigo wake wa samaki.
Wakati anaingia katika gari lake aina ya GX 100 alikutana na mlio wa simu yake, ilikuwa namba mpya, aliitazama kisha akabonyeza kitufe cha kupiga. Simu ikaita kidogo ikapokelewa na sauti nyembamba ya kike.

“Hassan jamani…nimekupigia simu muda mrefu kweli!!!”
“we nani??”
“Jamani mi Beaty!!!”
“Beaty yupi tena”
“Wa facebook…”
“aaah!! Beatrice wa Mwanza eeeh!!”
“Ndio mimi, tupo Mbezi vipi unakuja kunipokea kweli?”
“Poa nakuja!!” alijibu Hassan upesi. Kisha akafanya upesi
akakabidhi biashara yake kwa vijana wake akaingia garini akawasha gari na
kutokomea kwa kupitia njia za panya hadi akafika Ubungo stendi.
Zilikuwa zimepita dakika tano tangu gari la Zuberi kutoka Mwanza
liingie hapo stendi na kushusha abiria. Beatrice hakuwa na uhakika kama Hassan
atakuja kweli ama la!!! Aliposhuka akajaribu kuipiga simu ya Hassan haikupokelewa,
akajaribu tena haikupokelewa akaanza kukata tamaa. Akiwa anatafuta uwezekano
mwingine wa kutoka pale stendi mara simu yake ikamwonyesha kuwa Hassan alikuwa
anapiga. Akapokea haraka haraka. Kabla hajaongea simu ikakatwa, akahisi Hassan
amebip, akapiga kite cha karaha, akatazama salio kisha akataka kupiga.
Akashtukia ameguswa begani, alipogeuka akakutana na sura ngeni kabisa ikamtupia
tabasamu, hakujibu lile tabasamu badala yake akashangaa.
“Hassan Tembo…..” akajitambulisha kwa jina lake analotumia kule facebook.
“Mambo!!!” alisalimiwa katika hali ambayo ilionyesha kuwa Beatrice bado alikuwa katika mshangao.
“Poa…vipi za safari pole sana na karibu Dar”
“Asante mh!! Yaani kule facebook unaonekana mkubwa kweli mh!! Facebook ina mambo” Beatrice aliyasema hayo kwa kebehi. Maneno hayo yakamuumiza Tembo, akahisi amedharauliwa sana, lakini kabla ya kujibu chochote alimtazama kwa kuibia ibia Beatrice kuanzia chini, akakutana na viatu vyenye mtindo wa kisasa lakini vikiwa vimechakaa kutokana na kuikanyaga sana lami na kuvaliwa mara kwa mara, bila shaka hakuwa na viatu vingi, gauni lake kwa mahesabu ya haraka haraka lilikuwa halifiki hata shilingi elfu kumi na tano, kichwani alikuwa na wigi huku nywele zake halisi zikichungulia kwa mbali na kuutangaza uchakavu wake.
Mkononi alikuwa na mabangili ya bei chee huku akiwa amevaa na kicheni kilichopauka kikiwa na maneno I LOVE U…usoni hakuwa na mng’aro wa utajiri huku mkoba wake uliochakaa ukiutangaza umasikini wake kama sio ubahili.
“Mh!! Hana lolote huyu hebu ngoja…sijui na yeye nimwambie kuwa picha zake za facebook anaonekana mrembo?? Yaani anaonekana ana pesa kumbe hana maana yoyote” alijisemea Tembo huku usoni akizuga kutabasamu.

“Kwa hiyo unaelekea wapi sasa hivi, twende basi”
“Mh!! Asante Hassan usijali na asante kwa kuja mi nishafika
hivyo, tutaonana facebook baadaye basi!!” Beatrice alijaribu kumkwepa Tembo,
naye akaligundua hilo. Moyoni mwake aliitambua dharau ya Beatrice akaahidi
kumkomesha na kumkata kidomo domo.
“Wapi sasa unaelekea sasa hivi!!” Tembo aliuliza huku akijua
fika kuwa yule binti hakuwa na pa kwenda.
“Nitaenda hapo Magomeni ila kuna mtu namsubiri”:.alijibu.
“Basi twende nikusindikize!!”
“Nitaenda hapo Magomeni ila kuna mtu namsubiri”:.alijibu.
“Basi twende nikusindikize!!”
“Asante Hassan..usijali hata” alizidi kukwepa Beaty.
“Poa basi ngoja mi nirejee maskani yangu” alisema Tembo.
“Poa basi ngoja nikusindikize kidogo” Beaty akawa amejibu bila
kujua kuwa amefanya kosa kubwa sana. Walisogea mbele kidogo, Hassan mtoto Mama
Tembo akatoa funguo za gari akabonyeza. Gx 100 ikapiga kelele za kujitoa loki,
akafika akaegemea ile gari akaanza kuagana na Beaty tena. Wakati huu sasa Beaty
akatoa tabasamu la ukweli. Mara akawa muongeaji sana. Tembo akajua tayari
amemuingiza kwenye kumi na nane.
Wasichana kwa tamaa!!!
Lakini hakujua Beaty anajiingiza katika domo baya wakati huu!!
Wasichana kwa tamaa!!!
Lakini hakujua Beaty anajiingiza katika domo baya wakati huu!!
“Mh!! Huyu shoga yangu mwenyewe sijui haji??” Beaty akaanza
kujiongelesha ilimradi tu kufikisha ujumbe. Tembo akamwambia kuwa kama haji
waondoke naye, binti akaingia mkenge akakubali, milango ikafunguliwa, akakutana
na marashi ya aina yake huku mziki ukisikika kwa mbali sana kutoka katika
santuri iliyokuwa katika redio, hiyo ni baada ya gari kuwashwa. Beaty
akabweteka katika siti ya nyuma, Tembo akakataa kuendesha gari hadi alipohamia
siti ya mbele. Safari ya kutoka ikaanza.
Tayari Beaty alikuwa amesahau kuwa alisema kuwa Tembo ni mdogo
sana, sasa alikuwa anamwona kuwa ni mkubwa tena mtanashati. Tembo alikuwa kimya
sana huku akitikisa kichwa kufuatana na mdundo wa mziki uliokuwa unaendelea.
“B twende tukapate msosi kwanza au vipi”
“Poa tu twende” alikubali haraka haraka Beaty. Tembo akafurahi
na nafsi yake.
“Atanikoma na hatanisahau!!!” aliapa kimya kimya Tembo huku
akiiendesha gari kuitafuta Kinondoni. Na hatimaye akaifikia Best Bite, akapaki
gari wakaingia katika mgahawa ule maarufu jijini Dar es salaam.
“Chipsi mayai….” Akaagiza B, muhudumu akamwambia hakuna orodha hiyo ya chakula. Tembo akacheka kimoyo moyo akagundua kuwa Beatrice alikuwa na ujanja wa facebook tu, wala kimaisha halisi hakuwa na ujanja wowote. Hata chakula kilivyoletwa Beatrice hakujua jinsi ya kutumia uma na kisu , kuzitumbua chipsi na paja la kuku lilokuwa mbele yake.
Kwa mara nyingine tena Tembo akausoma ushamba wa Beatrice!!!!
Kwisha habari yake!!!!!! Akajisemea huku akistaajabu huo ujasiri alikuwa ameutoa wapi.

**Nani ni mwajiriwa kutoka kuzimu????
**Je? Hassan Tembo atafanikiwa azma yake na kwanini anasema kuwa atamkomesha Beatrice.
**Nchi ya bluu ni ipi???
**Je? Hassan Tembo atafanikiwa azma yake na kwanini anasema kuwa atamkomesha Beatrice.
**Nchi ya bluu ni ipi???
Simulizi imeanzia hapa…..Kama kawaida…
SIMULIZI HII Itakuwa ikikujia saa mbili asubuhi kila siku
SIMULIZI HII Itakuwa ikikujia saa mbili asubuhi kila siku

0 comments:
Post a Comment