Kumekuwa na majibizano ya hapa na pale kati ya rapper Nay wa Mitego na aliyekuwa producer wa studio yake ya Free Nation Mr T-Touch ikiwa ni baada tu ya wawili hao kutofautiana na kila mmoja kufanya kazi kimpango wake.
Mengi yamesikika kutoka kila pande lakini leo hii Mr T-Touch amepaza sauti na kipaza cha Perfect255 na kujibu kauli ambayo aliizungumza Nay wa Mitego eti kwamba studio mpya ya producer huyo sio yakwake bali anaishi nyuma ya migongo ya watu.
“Nay ni lazima azungumze hivyo kwasababu yeye ni mtu ambaye huwa haamini kwenye mafanikio ya mtu, Nay huwa anaamini kwenye mafanikio yakwake peke yake. Kwahiyo hawezi kuizungumzia hiyo vizuri kwasababu ni kitu ambacho kinam-pain.” Aliongea Mr T-Touch.
Unaweza kumsikiliza Mr T- Touch akituma ujumbe mzito kwa rapper Nay wa Mitego kwa kuplay hii video hapa chini.
0 comments:
Post a Comment