Wednesday, January 4, 2017

Katibu tawala mkoani Kagera Diwan Othman, amemuagiza mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba kuwasimamisha kazi mara moja watumishi watatu waliokuwa wakisimamia ukarabati wa shule ya sekondari ya Omumwani iliyokarabatiwa kuhamishia wanafunzi wa Ihungo kwa muda.
Watumishi hao ni mhandisi mkuu wa manispaa ya Bukoba Andondile Mwakitalu, msanifu majengo Charles Kafumu na mhandisi msaidizi Felix Costantine, huku akimtaka mkurugenzi ateue wengine kusimamia ukarabati wa shule hiyo.
“KATIBU TAWALA KAGERA
Ametoa uamuzi huo baada ya kupewa maagizo kutokana na ziara ya rais Magufuli aliyejionea namna ukarabati ulivyofanyika usivyo wa kuridhisha.Mhandisi Andondile akijieleza kwa katibu tawala mkoa wa Kagera
Amesema kuwa makabidhiano yafanyike leo hii ili kesho mkurugenzi wa mansiapaa amkutanishe na wahandisi wapya aliowachagua kwa lengo la kuendeleza mchakato huo.
Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba Chibhunu Lukiko,Kaimu mkurugenzi akitoa ufafanuzi mbele ya maofisa wa manispaa.
amesema kuwa fedha zinazotajwa kupotea kutokana na kazi ndogo iliyofanyika, ni milioni 119 ambazo zilikuwa zinatajwa kuwa zimelipwa ilhali kuna baadhi ya vibarua ambao bado hajawalipwa.

Sambaza hii:

0 comments:

Post a Comment