Thursday, February 2, 2017

Kwenye teaser ya kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz cha Salama Jabir kinachoruka kila alhamis saa 3 usiku kupitia EATV, Abdu amewakumbusha mastaa Alikiba na Diamond kuwa nyuma yao kuna vijana wenye hasira wanaozitafuta nafasi zao.

“[Alikiba na Diamond] waamini kuwa wapo watu wamejipanga kwaajili ya kuweza kuwatoa kwenye nafasi zao, wapo wengi ambao wana uwezo wa kufanya hivyo, nadhani bado hawajafikia muda,” anasema Abdu.
Unakubaliana naye? Unadhani kuna siku watakuja kujitokeza wasanii watakaokuwa na nguvu sawa na Kiba na Chibu? Ukichekecha akili muda huu, ni wasanii gani waliopo sasa wanaonesha dalili za kuelekea huko?

0 comments:

Post a Comment