Wednesday, February 8, 2017

Mchekeshaji na mshindi wa shindano la BBA 2014, Idris Sultan amefunguka kupitia ukurasa wake wa Instagram juu ya ile sauti ya Wema iliyorekodiwa bila ya Wema mwenyewe kujua.

Sauti (clip) hiyo ambayo anasikika mwanadada Wema Sepetu akielezea kila kitu juu ya kile kilichodaiwa kuendelea kwenye sakata la madawa ya kulevya na kutoboa siri nzito ambayo wengi walikuwa hawaifahamu hapo awali!
Idris amefunguka kwa wanaokwenda kumtembelea Wema wengi ni wanafiki na wanamalengo yao mengine tofauti na kwenda kumjulia hali Wema. Mpaka hivi sasa sakata hili bado linaendelea kupata sura mpya na kuwa gumzo zaidi nchini.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Idris aliweza kuuandika ujumbe huo na kwa bahati mbaya haukuwa na uhai mrefu, ukatolewa (post ikafutwa). ila Perfect255 iliweza ku-screenshot ujumbe huo.
Idrisa-Sultan
Ujumbe huo ulisomeka hivi.. “Na muendelee kupiga kulele kutembelea watu central na recording people bila wao kujua. Kwakua tunachukulia maisha ya watu kama mfumo wa likes na following bila tunawaumiza kiasi gani kwa tunachokifanya basi let us proceed na tutaona kama tunaowapenda kama tunavyosema tutakua tumewatendea haki.
Aliongeza, “Kwa hili nimeshindwa kunyamaza you claim to be friends and true people kumbe unafiki unatujaa. We will kill our families and be the 1st to cry kwenye Msiba WHERE IS HUMANITY? kama hamjapenda kutoa moral support basi kaeni majumbani kwenu na mposti posti vimachozi na unafki wenu sio hata pale pasafi padogo palipo baki”.

0 comments:

Post a Comment