Ndama wa ajabu amezaliwa nchini New Zealand akiwa na miguu 8,masikio 4, miilimiwili,masikiomanne
Mmiliki wa ndama huyo, Neil Davy,ambaye amemshika ndama huyo aliyekufa kwenye picha aliuambia mtandao wa NZ wa nchini humo kuwa kama yeye asingekuwepo wakati ndama huyo akizaliwa basi ng’ombe aliyemzaa ndama huyo naye angekufa kwani alihangaika sana wakati akizaa.
‘Ilikuwa
ni vigumu kumuangalia wakati alipokuwa anazaa,kwani hali yake ilikuwa
mbaya sana alikuwa akipiga kelele kutokana na maumivu aliyokuwa
akiyapata kutokana na ndama mwenyewe alivyo nilihangaika naye sana hadi
nikalowa jasho jingi,’’alisema Davy.
Davy
aliongeza kuwa alidhani ng’ombe huyo angezaa mapacha lakini kutokana na
sababu ambazo hajazifahamu kikazaliwa kiumbe cha ajabu kama hicho.
0 comments:
Post a Comment