Mlinzi wa kati wa klabu ya Simba SC, Method Mwanjale amekabithiwa Shilingi milioni moja mara baada ya chaguliwa kuwa mchezaji bora Desemba wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2016/2017.
Katika mwezi huo Mwanjale aliiwezesha Simba kushinda mechi zote tatu, hivyo timu yake
kupata ushindi wa asilimia 100 kwa kunyakua pointi zote tisa.
Wachezaji wengine walioshinda tuzo za mchezaji bora kwa msimu wa
2016/2017 hadi sasa ni John Raphael Bocco wa Azam (Agosti), Shiza
Ramadhan Kichuya wa Simba (Septemba), Simon Happygod Msuva wa Yanga
(Oktoba), na Rifati Hamisi wa Ndanda (Novemba).

0 comments:
Post a Comment