Wednesday, February 15, 2017

Klabu ya soka ya Arsenal inamtihani wa kuhakikisha inaska matokeo katika mchezo wa ugenini dhidi ya miamba wa soka nchini Ujerumani, klabu ya Beyern Munich. 


Kuelekea katika mchezo huo Meneja wa klabu ya Beyern Carlo Ancelotti, amesema ili kushinda katika mchezo wa ligi ya mabingwa ni lazima kujitoa na uwe na bahati pia.


Ancelotti amesema kikosi chake kitahakikisha kinamiliki mpira na kutokuruhusu kufungwa bao.

Nae meneja wa klabu ya Arsenal, kikosi chake kitaingia katika mchezo wa leo kikiwa kimesahau michezo iliyopita kwani jambo kubwa lililopo mbele yao ni kuhakikisha wanapata matokeo.


Wenger amesema klabu yake ina faida kubwa kwani imeanzia ugenini na itamalizia nyumbani.

Katika hatua nyingine Wenger amesema anawaheshimu sana Bayern lakini ni lazima kikosi chake kipambane ili kiweze kupata matokeo.

0 comments:

Post a Comment