Billnass ni mmoja kati ya mastaa ambao mara kwa mara wamekuwa wakihusishwa kutoka kimapenzi na mastaa wa kike hapa Bongo.
Ikiwa Linah, Shilole na hata Nandy ni baadhi ya mastaa wa kike ambao wamewahi kusikika kutoka kimapenzi na Billnass.
Sasa Billnass amepiga story na Perfect255 na amekanusha uvumi huo na kudai kwamba yeye hawezi kuyaweka mahusiano yake public kwasababu mahusiano yakiwa public kwa mtu maarufu kuna faida na hasara pia.
“Siwezi kuweka mahusiano yangu wazi kwasababu hii tasnia inaangaliwa na watu wa rika zote, kuanzia watoto, vijana mpaka watu wazima, sasa haitopendeza leo wakiona niko na mtu huyu halafu baada ya wiki siko naye kiasi kwamba hadi mwisho wa siku nakuwa nimeshatangaza mahusiano sita au nane, kitu ambacho sio kizuri. Me nataka Billnass akisikika yuko na mtu fulani hata kama itatokea bahati mbaya basi iwe ni mara mbili au mara moja.”
0 comments:
Post a Comment