Thursday, February 9, 2017

Image result for gwajima images

- Askofu mtata nchini Gwajima ambaye ametajwa kuhusika na bishara ya Madawa ya kulevya, leo alizungumza na Media kuhusu sakata lake hilo na kuwaacha wote wakiwa na kicheko cha ajabu soma aliyoyasema live!!;-


 Gwajima:- Namuomba Rais ambadilishie Kazi Makonda, hii ya Ukuu wa Mkoa kutawala na kuongoza hata watu usiowapenda imemshinda. Sisemi amfukuze hapana nasema ambadilishie Kazi.
Gwajima : Makonda ana chuki na wivu na mimi
Gwajima : alikasirika hata niliposhuka na helkopta yangu siku ya mechi ya viongozi wa dini na wabunge dodoma.
Gwajima : nilichelewa kidogo nikaamua kupanda helkopta yangu mpaka uwanjani kabisa.
Gwajima : mimi nilicheza namba kumi Makonda namba tisa, jicho alilokuwa ananiangalia ni la chuki mpaka nikawa nashangaa.
Gwajima : hii hapa picha niko na Makonda, naibu spika na viongozi wengine tukichangia ujenzi wa taifa mbona hajanikamata hapa kama ninauza unga? .
Gwajima : Makonda alikuja kanisani kwangu na marehemu sitta na akapanda mazabauni je hakujua kama nauza unga? .
Gwajima : hili ni shambulio kwa kanisa sio kwa Gwajima
Gwajima : hili ni shambulio kwa wote walio okoka tuonekane hatufai
Gwajima : hili ni shambulio kwa maaskofu wote na wachungaji wote
Gwajima : kwa sababu Gwajima ana kanisa kubwa
Gwajima : kwa sababu Gwajima ana waumini zaidi ya elf sabini kanisani kwake na makanisa zaidi ya 400 nchi nzima.
Gwajima : nilikuwa mkali Sana kwa serikali ya awamu ya nne na kikwete
Gwajima : nilikemea sana kupotea kwa ndovu kila siku
Gwajima; Makonda anafanya hivi kwa maslahi ya Nani? .
Gwajima : Makonda anafanya hivi kufurahisha serikali iliyopita ionekana nimekomolewa.
Gwajima : Hili ni shambulio kwa Ukristo. Rais wangu mpendwa mbadilishie Kazi Makonda.
Gwajima : Makonda hajatumwa na Rais kufanya anayoyafanya
Gwajima : mimi namfahamu vizuri Rais, hawezi kumtuma Makonda kufanya hivi.
Gwajima : Makonda atavuka mipaka sasa, atakemea Polisi, atakemea jeshi, atakemea wabunge
Gwajima : Makonda atakemea mpaka waziri mkuu.
Gwajima; wenzetu wabunge wameungana kutumia sheria na kanuni zao watamuhoji.
Gwajima : sisi raia wa kawaida tusio na sheria wala kanuni za kututetea tutashtaki wapi? .
Makonda ana chuki na Gwajima sio Bure.

0 comments:

Post a Comment