Mwenye Fulana nyekundu ndiye kijana aliyesambaza waraka uliowataja watu wengi maarufu kuwa wanaita Polisi hivi karibuni alipo onyeshwa na Kamanda Sirro leo live!!
Jeshi la Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetoa taarifa ya kukamatwa kwa jumla
watuhumiwa 349 katika oparesheni ya kuwasaka watu wanaohusika na dawa za
kulevya
Akizungumza leo
Jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,
Kamishna Simon Sirro amesema kati ya watuhumiwa hao, wamo wauzaji,
wasafirishaji na watumiaji wa dawa za kulevya, na kwamba wataanza
kufikishwa mahakamani siku ya kesho, huku mmoja akipandishwa kizimbani
leo.
Pia ametoa
taarifa ya kijana mmoja anayedaiwa kusambaza taarifa za uongo, ambapo
amesema kuwa jeshi hilo linamshikilia kijana huyo ambaye ni mwanafunzi
mwenye umri wa miaka 23, anayedaiwa kutaja majina ya viongozi na
kuwatuhumu kuwa wanahusika na dawa na dawa za kulevya.
Kuhusu askari 9
waliotuhumiwa kuhusika na dawa hizo, Kamanda Sirro amesema askari hao
wamekabidhiwa kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya kuzuia na Kupambana na
Dawa za Kulevya kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kamanda Sirro
amesema hadi sasa jumla ya kete 612 pamoja na bangi vimekamatwa na
kwamba kuna watu wengine 17 ambao bado jeshi hilo linawafuatilia na
watakuwa mbaroni wakati wowote.
|
0 comments:
Post a Comment