
Baadhi ya maofisa kutoka klabu ya Yanga na ofisini
kwa Mwenyekiti wao Yanga, Yusuf Manji walilazimika kubaki katika kituo
cha kati hadi usiku wa manane kwa kuwa hawakuwa wakijua Manji alikuwa
amepelekwa wapi.
Lakini baadaye alirejeshwa katika kituo hicho Kikuu cha Polisi cha Dar es Salaam, takribani saa sita usiku.
Baada ya Manji kurejeshwa na kuingizwa kituoni hapo, taratibu maofisa hao walianza kuondoka katika eneo hilo.
Kabla waliendelea kubaki hapo wakieleza walitaka kujua alipokuwa amepelekwa.
Manji pamoja an na Mchungaji Josephat Gwajima
walipakiwa kwenye gari la Polisi aina ya Toyota Landcruiser lenye rangi
nyeupe, ilikuwa kama saa 10 na nusu jioni.
Gari hilo lenya usajili namba T 213 ARS liliondoka
kituoni hapo kuelekea Posta ya zamani na haijajulikana hadi sasa
walipelekwa wapi na hawakuwa wamrejeshwa kituoni hapo.
Source:- ChoiceTZ Blog
0 comments:
Post a Comment