
MATEJA WAWILI WAFARIKI KWA KUKOSA DAWA ZA KULEVYA
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga amesema watu wawili wameripotiwa kupoteza maisha mkoani Mwanza kwa sababu ya kukosa dawa za kulevya mtaani kama walivyozoea.
Kamishna Sianga amesema taarifa hiyo ameipata kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, hali inayomaanisha mafanikio ya mapambano ya dawa hizo, ambapo kwa sasa usambaaji wake umepungua mtaani kwa kiasi kikubwa.
"Nimeongea na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, ameniambia kwamba kuna watu wawili wamefariki sababu walikuwa drug addict na sasa dawa hizo hazipo mtaani" amesema Sianga.
Maneno Yangu.
Serikali iongeze dawa za methodine katika mahospitali ya serikali ili kuweze kuwepo na mbadala wa dawa za kulevya kwa viwango ili waweze kupewa waathirika ili baada ya muda waachane nayo.
Bila hivyo basi tusubirie mizogo mingi mtaani na halmashauli zetu zimetangaza kuwa maeneo ya kuzikia yamekwisha.

0 comments:
Post a Comment