Posted by Williammalecela.com on Thursday, February 16, 2017
 |
JESHI la polisi Mkoani Mbeya, linamshikilia mfanyabiashara maarufu
Jijini Mbeya, Steven Samweli (Maranatha), kwa tuhuma za kujihusisha na
biashara za dawa za kulevya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari alisema kuwa
Maranatha, alikamatwa juzi, kwenye moja ya duka lake la biashara za dawa
baridi kwa matumizi ya binadamu.
Alisema, baada ya polisi kupata taarifa za kuhusishwa kwa
mfanyabiashara huyo na mtandao wa dawa za kulevya, liliweka mtego na
hatimaye kufanikiwa kumtia nguvuni na sasa anahojiwa.
Aidha, kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo, kunafikisha idadi ya watu
nane wanao tuhumiwa kujihusisha na uingizaji, usambazaji na utumiaji wa
dawa za kulevya Mkoa wa Mbeya, huku watumiaji wanaoshikiliwa wakiwa ni
23.
Credit Fahari news |
0 comments:
Post a Comment