Tuesday, February 21, 2017

Moja kati ya issue zilizokuwa zikitrend mitandaoni asubuhi hii ni Jokate kuonekana pichani na wakali wa muziki kutoka Marekani, Jay Z, Beyonce na Remy Ma.
Picha hiyo iliyopigwa kwenye Mechi ya mpira wa Kikapu ya NBA All-Star Game Jokate alionekana akijibizana kitu na Jay-Z huku Mtoto wao Blue Ivy akiwa anamtazama Jokate kwa karibu sana, ambapo ilizua maswali mengi ni vitu gani walikuwa wanaongea?
Anyway.. Picha hiyo haikuwastusha tu mashabiki wake bali hata mastaa pia wali guswa kwani sio jambo la kawaida kukutana na Wasanii wakubwa kama wale na kuongea nao au hata kupiga picha nao. Baadhi ya mastaa walioweza kuonyesha hisia zao mara baada ya kuona picha hiyo ni Shilole na Godzilla.
Shilole
Ujumbe huo kutoka kwenye ukurasa wake wa Instagram ulisomeka hivi.. “Jojo wangu weeeeeeeeeeeee umeenda kwa my Dady trump hongera sana naona uko na familiya ya J Z na beyonce dada weweeeee big up @jokatemwegelo usiondoke unisubir nakuja kwa Dingi”
GodZilla

Tweet hiyo kutoka kwenye akaunti yake ya Twitter ulisomeka hivi.. “Haki mungu nimeota hii …i swear… Malaika wangu nomaaa” hii ni baada ya kuona tweet ya Jokate.

0 comments:

Post a Comment