Model wa Tanzania anayefanyia kazi zake nchini Afrika Kusini, Daxx Cruz,aweka wazi vigezo vya mtu anayestahili kuwa mwanamitindo ‘model’, na kutaja baadhi ya ‘models’ wa Bongo wasiokuwa na vigezo.
Daxx amemtaja model anayefahamika kwa jina la Calisah ambaye siku za karibuni alijipatia umaarufu baada ya kutangaza kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mrembo Wema Sepetu, kuwa hastahili kabisa kufanya kazi hiyo kwa kuwa hana vigezo.
Kuhusu models wa kiume adai “Upande wa models wa kiume, siwajui, mi nawaonaona tu, mtu pekee nayemkubali anaitwa Abel, saizi yuko South Afrika, lakini wengine wapowapo tu….” Alisema katika kipindi cha KIKAANGONI kinachoruka LIVE kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV.
Daxx Cruz
Alipotajiwa majina ya models watatu (Rota, Calisah na Mario, haya ndiyo yalikuwa majibu yake… “Rota Molel ana muonekano mzuri lakini ana attitude, kile ndicho kinachomuangusha, ni model mzuri lakini atitude… Calisah NO, ni mfupi, for me No, labda kw Tanzania, unajua model siyo kuwa na six packs, akija South hapati kazi… Mario (ambaye amewahi kuwa Mr. Tanzania, kwangu No”
Mwingine ambaye hana vigezo, Daxx amemtaja mwanadada Hamisa Mobeto kuwa hastahili kuwa ‘model’ kwa kuwa amekaa kiurembo zaidi na kwamba anafaa kwa kazi ya kuonekana kwenye video za miziki (Video Vixing) hivyo kutokidhi vigezo vya kimataifa vya kuwa ‘model’ labda kwa Tanzania.
Amewataja baadhi ya watu ambao anadhani kuwa ni ‘models’ wazuri na ambao endapo watakaza, watafika mbali kuwa ni pamoja na Nelly Kamwelu kama mtu anayemkubali huku akitaja kasoro kubwa inayowakwamisha wadada wengi Tanzania.
“Wadada wengi wako fresh, tatizo wanajiachia.. wanafanya maisha ya uanamitindo kuwa kitega uchumi”
0 comments:
Post a Comment