Ikiwa leo ni siku maalum kwa wapendanao duniani, nikiwa namaanisha Valentine’s Day hitmaker wa ngoma ya Kidebe Abdul Kachaa almaaruf kama Dogo Janja amefunguka yakwake ya moyoni kumuhusu staa wa Bongo Movie Irene Uwoya.
Dogo Janja ameiambia Perfect255 kuwa mmoja kati ya watoto wazuri ambao toka kitambo huwa wanamnyima usingizi ni mrembo Irene Uwoya. Na kudai kuwa anatamani sana siku moja aweze kummiliki hata japo kwa usiku mmoja tu.
“Irene Uwoya nampendaga tangu niko mtoto, nimesha bandika sana picha zake magetoni, nampendaga sana na hii sio mara ya kwanza kuongea kwenye media, ni mtu ambaye nammezeaga mate kinyama.” Alisema Dogo Janja.
Dogo Janja hakuishia hapo tu, yapo mengi amefunguka kuhusiana na mrembo huyo wa Bongo movie. Full Interview nimekuwekea hapa kwenye video hii hapa chini. Bonyeza play kumsikiliza Janjaro Republic Nyang’au.
0 comments:
Post a Comment