Saturday, February 11, 2017


MTANZANIA ambaye makazi yake yapo Nchini London Farid Jan Mohamed lakini yeye hupenda kujiita Fuad Jamal a.k.a ( Mzee baba),amefikishwa Mahakama ya mwanzo Kariakoo kwa tuhuma  za kutumia lugha ya matusi mtandaoni ambapo akiwa huko london  alijirekodi kwa njia ya whatsup  kwa kumtukana matusi makubwa mama yake mdogo na kuyasambaza mtandaoni katika nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania.


Akisoma mashtaka hayo mwishoni mwa wiki  Karani Blanka Shayo, mbele ya Hakimu Matrona Luanda alisema mshtakiwa litenda kosa hilo Desemba 3 mwaka jana akiwa nnchini London kwa kusambaza ujumbe wenye sauti yake akimtukana mama yake huku akijua ni kosa kisheria.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo Mshtakiwa alipoiulizwa alikili kutenda kosa hilo ambapo Hakimu alimtaka Mlalamikaji aeleze namna ilivyokuwa na alivyopokea ujumbe huo .

Mlalamikaji alisema Desemba 3 mwaka jana akiwa amekaa ofisini ujumbe uliingia kwenye simu yake na alipoufungua ilikuwa ni sauti ya matusi makubwa yakimtaja yeye na watoto wake na baada ya muda watu tofauti walianza kumpigia simu ikiwemo wafanyakazi wenzie kumuuliza wamesikia ujumbe wa matusi ukisambaa na ukimtaja yeye.

"Mshtakiwa ni mtoto wa dada  yangu  kabisa na ni kama mtoto wangu   ila nashangaa kwanini alinidharirisha kwa matusi makubwa ambapo nimepigiwa simu kutoka Air Tanzania, Thailand, China na watu wengine wengi wakiniuliza mbona ujumbe wa matusi makubwa unasambaa na ukinitaja mimi imeniumiza sana" alisema Delila.

Hakimu alimtaka Mshtakiwa aeleze Mahakamani kwanini amemtukana mama yake matusi makubwa kama hayo ambapo na yule ni kama mama yake jambo ambalo alisema ni tabia mbaya mbaya na ya ajabu sana katika utamaaduni wa Kitanzania.

" Muheshimiwa kweli huyu ni mama yangu mdogo mimi ndio mtoto mkubwa kwetu yeye amekuja kuingia nyumba ya mama yangu kutaka kuiuza ndo nikachukua jukumu hilo na lainisema nimerudio Tanzania kwa kuwa wanaume Ulaya wamenichoka hivyo nakuja kutafuta wa Tanzania" alisema Mzee Baba.

Hakimu alimuuliza Hakimu kama kuna kumbukumbu za nakosa ya nyuma za mshtakiwa abapo alisema hakuna ila apewe adahabu iwe fundisho kwa wengine na wenye tabia kama zake.

Luanda alimwambia mshtakiwa ajitetee kabla ya adhabu ambapo alisema yeye Tanzania hana pakuishi alifikia hotelini  na tiketi yake ya ndege imeisha mda mama yake haongei naye na anaishi tu kwa marafiki anaomba apunguziwe adhabu aweze kutafuta nauli ya kurudi ulaya.

Hakimu  alisema mshtakiwa anatakiwa kulipa faini ya sh. 50,000 kwa siku hiyo na akishindwa aende jela miezi sita na akiweza kulipa faini aende kuomba msamaha kwa mama zake kwa laichokifanya na asirudie tena.

Hata hivyo Mshtakiwa huyo mwaka jana Desemba  alizuliliwa  uwanja wa ndege wa  Tanzania akiwa anarudi London akiwa na babu wa kizungu aliyekuja naye   kutokana na kesi hii ambapo Mzungu  aliondoka na yeye kubaki nchini.

0 comments:

Post a Comment