![]() |
| Mchezaji wa klabu ya Leicester City, Andy King akiiandikia klabu yake bao la kwanza. |
Hatimae
klabu ya soka ya Leicester City imefanikiwa kupata ushindi wake wakwanza ndani
ya mwaka 2017 ni mara baada ya kuibamiza Derby
County kwa kichapo cha mabao 3-1.
Katika mchezo huo wa raundi ya nne katika FA Cup uliopigwa
katika dimba la King Power Stadium Leicester ilipata bao la kwanza katika
dakika ya 47 mfungaji akiwa ni Andy King.
Mara baada ya bao hilo kupatikana Derby
Contry ilipambana na kusawazisha bao hilo katika dakika ya 61 mfungaji akiwa ni
Abdoul Razzagui.
Mabao mengine ya klabu ya Leicester
City yalipachikwa na Onyinye Ndidi na Damarai Gray. Mabao hayo yalipatikana katika
dakika za nyongeza mara baada ya mchezo huo kulazimika kufika katika dakika
120.
Sasa Leicester itashuka tena dimbani
February 18 kukipiga dhidi ya Millwall katika hatua ya 16 bora.



0 comments:
Post a Comment