Posted by Williammalecela.com on Monday, February 13, 2017
 |
MANENO YA TID LEO LIVE KUHUSU VITA YA MADAWA YA KULEVYA!!:-
Mh. Mkuu wa Mkoa Mh. Commissioner Siro Ndugu waandishi, assalam aleykum!
Naomba kujitambulisha naitwa Khalid Mohamed na ni nimekuwa muathirika wa madawa ya kulevya.
Leo hii siko hapa kutoa historia kwanini, ilikuwaje nikaingia kwenye
matumizi ya madawa ya kulevya hayo naomba tuweke kwa siku nyingine.
Nimekuja mbele yenu hapa kama kijana aliyepotea njia hapo nyuma na
kuingia katika janga hili la taifa, kutoka moyoni mbele yenu nyinyi
waandishi, Mh RC na wote wanaotazama na kusikiliza huko manyumbani
kukiri nilikosea sana familia, mama yangu marafiki na jamii kwa ujumla
na pia kuchukua fursa hii kuwaomba msamaha wale wote niliowakwaza when I
was under drug influence. I pray that you all forgive me.
Nimesimama hapa kama kijana shupavu, mpambanaji, mwenye nguvu mpya
lakini pia niko hapa mbele yenu kama "Mnyama" na niko tayari kuunga
mkono vita hii ya madawa ya kulevya narudia tena "Mnyama" manake vita
hii inabidi uwe mnyamaaa kama kakangu Makonda ili kuishinda.
Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Kakangu Mh Makonda, najua
wengi wanajiuliza imekuwaje kwanini? Lakini hakuna anayejua nimepitia
mangapi mpaka kufikia hapa, labda nilihitaji nguvu ya dolla itumike ili
nione uzito na ukubwa wa hili jambo. Nakushukuru wewe binafsi Kakangu
Makonda, Mh Raisi kwa kutuamsha sisi vijana na kuona kwamba hata
serikali iko tayari kutusaidia kutokomeza shetani huyu, this is a wake
up call for me sitorudi nyuma kamwe. Natangaza rasmi kujiunga katika
vita hii naomba M/Mungu atuongoze tuokoe maisha ya vijana wenzangu huko
mitaani.
Naamini Muziki bila madawa inawezekana!!!!
Asanteni sana.....
|
0 comments:
Post a Comment