Serikali ya Hungary imethibitisha kwamba jiji la Budapest limejitoa katika mchakato wa kutaka kuhodhi michezo ya olimpiki ya mwaka 2024.
Budapest imejitoa kufuatia shinikizo la zaidi ya watu 260,000 waliotia saini ya kupinga mpango wa kuandaa michezo hiyo wakidai kuwa maandalizi ya michezo hiyo ni uchezeaji wa pesa za wananchi.
Wananchi hao wameitaka serikali kutumia fedha ambazo wangezitumia katika maandalizi ya michezo hiyo kwenye maendeleo ya mashule pamoja na hospitali.
Msemaji wa serikali ya Hungary Zoltan Kovacs amelieleza shirika la utangazaji la Reuters kwamba maamuzi yaliyofikiwa na serikali yametokana na mazungumzo yaliyofanyika baina ya Waziri Mkuu Viktor Orban, Meya wa jiji la Budapest - Istvan Tarlos pamoja na kamati ya Olimpiki ya Hungary.

0 comments:
Post a Comment