Huwezi kutaja wasanii ambao wamechangia kupeperusha bendera ya muziki wa kizazi kipya duniani bila kutaja jina la ‘Nassib Abdul’ maarufu kama Diamond Platnumz.
Hoja za kununua watazamaji katika mtandao wa Youtube zilichukua nafasi miezi kadhaa nyuma kati ya Ommy Dimpoz na Diamond Platnumz. Hoja zao zilifika mbali hata kupelekea kutoleana kauli zisizofaa mbele ya mashabiki kupitia mitandao ya kijamii na media kwa ujumla.
Lakini pia mashabiki na wasanii wanapaswa kujua kuwa hakuna jambo baya kununua watazamaji katika mtandao wa Youtube, ni katika hali ya kujitangaza zaidi kwa kutumia fursa ya mtandao. Jambo baya ni kudangaya kuwa watazamaji hao msanii anawapata kwa hali ya kawaida sio ya kununua kwa maana ya “Kupromote”.
Wimbo wa ‘Marry You’ wa Diamond Platnumz aliyomshirikisha Neyo ni kielelezo cha kununua watazamaji, ikiwa na maana ya kupata watazamaji wengi katika muda mfupi.
Wimbo huo umekuwa ‘Promoted’ kwenye mtandao wa Youtube kama tangazo ili uweze kupata watazamaji wengi kwa wakati mfupi. Hivyo unapoingia tu katika mtandao wa Youtube ni lazima ukutane na wimbo huo.
0 comments:
Post a Comment