Monday, February 6, 2017

Umeshawahi kufikiria kuhusu Dogo Janja kuwa na lebo yake mwenyewe kisha msanii wa kwanza kumsainisha akawa ni ya Young Killer? Sasa fikiria itakuwaje endapo ikitokea.

Msanii Dogo Janja kutoka kundi la Tip Top Connection amekuwa na Ndoto siku moja ya kuja kumiliki Lebo yake ya Muziki kama Wasanii wengine wakubwa wanavyofanya.
Dogo-Janja-681x851 (1)-horz
Dogo Janja & Young Killer
Siyo jambo la ajabu kuona msanii aliyetoka kimuziki kumsaidia msanii mwenzake au kumsimamia msanii mwenzake ili aweze kufanikisha ndoto zake kwani hata wasanii wanaotajwa kuwa wakubwa duniani  nao pia wanasimamiwa na wasanii wenzao mfano RihanaKanye West  na wasanii kibao wanasimamiwa na lebo ya Jayz inayokwenda kwa jina la Roc Nation.
Kupitia kipindi cha Friday Night Live (FNL), Dogo Janja adai endapo angekuwa tayari anamiliki lebo yake na msanii wa Kwanza aliyemtaja kumsaini kwenye Lebo hiyo angekuwa ni Young Killer.
Dogo Janja anaekonga nyoyo za mashabikli wake na wimbo wake wa ‘Kidebe’, alisema “Young Killer ni msanii mkali  lakini anahangaika sana kutoboa hivyo angemsaini ili kufikia malengo yake”.

0 comments:

Post a Comment