Source: Jamii Forum
Kupitia clip ya mazungumzo ya sauti iliyovuja kati ya mama Wema Sepetu na Steve Nyerere mambo mbalimbali yajulikana ambayo ni pamoja na mbinu kadhaa zilizofanyika ili kumuokoa Wema Sepetu na janga zima la dawa za kulevya.
kutokana na clip hiyo inaeleza kuwa Bw, Steve Nyerere, ndiye mtu aliyefanya jitihada kubwa zaidi kumuokoa Wema Sepetu ikiwemo ni pamoja na kwenda bungeni mjini Dododma ili kuzungumza na baadhi ya viongozi wakiwemo, Mwigulu Nchemba, ambae ni waziri wa mambo ya ndani, mbunge wa geita mjini alimaarufu kama Msukuma, waziri wa sanaa na Michezo, Mhe, Nape Nauye, makamu wa rais mama Samia Suluhu Hassani pamoja na wengine wengi aliowaorodhesha katika mazungumzo yake hayo.
steve anasema kuwa Nape na kundi lake walipanga kumpigania Wema pasipo yeye kujua kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kuepuka uropokaji wa Wema kwani hawezi kutunza siri.

0 comments:
Post a Comment