Thursday, February 9, 2017



Mcheza teniss Heather Watson na Johanna Konta wamefanikiwa kupata ushindi katika michezo yao ya awali na kuipa Uingereza ushindi wa 2-0 katika michuano ya Fed Cup inayoendelea huko Estonia Estonia.


Konta anaeshikilia nafasi ya 10 kwa ubora duniani amefanikiwa kupata ushindi wa seti 6-2 6-3 katika tatu bora dhidi ya Jelena Ostapenko anaeshikilia nafasi ya 34 kwa ubora duniani.

Kwa upande wa Watson, anaeshikilia nafasi ya 72, amemshinda Diana Marcinkevica anaeshika nafasi ya 306 kwa seti 6-3 6-0 ndani ya dakika 61.

0 comments:

Post a Comment