Miongoni mwa vipimo vya video ya muziki kupokelewa vizuri ni pamoja na namba za watu waliotazama au kupakua mtandaoni. Kwa kutumia kigezo hicho video ya ‘kidebe’ imepenya.
Video ya wimbo wa Dogo Janja ‘Kidebe’ imefanikiwa kufikisha views milioni moja kwenye mtandao wa Youtube. Speed hii inaweza kuifikisha mbali zaidi video hii ambayo ilianza kuonesha mafanikio makubwa mara baada ya kuachiwa na kuifanya kuwa video ya Dogo Janja iliyotazamwa zaidi kati ya video zake zote.
Kupitia mtandao wa Instagram, Dogo Janja ameandika, “The best is still yet to come.. #1MillionViews
”
Mpaka sasa ni miezi 5 imepita tangu video hiyo ilipowekwa kwenye mtandao huo mwezi 8 mwaka jana na imefanikiwa kutazamwa mara 1,000,735.
0 comments:
Post a Comment