Wednesday, February 22, 2017


Mlinda mlango wa klabu ya Sutton United Wayne Shaw amelazimika kustaafu kucheza soka akiwa na umri wa miaka 45 amethibitisha kocha wake Paul Doswell.


Shaw, amelazimika kutundika daluga kutokana na kashfa ya kubashiri matokeo ya mchezo wa kombe la FA ulioikutanisha klabu yake ya Sutton United dhidi ya Arsenal.
Mchezo huo ulikamilika kwa Arsenal kupata ushindi wa mabao 2-0 mabao hayo yakipachikwa na mwanandinga Lucas Perez pamoja na Theo Walcott.

Katika mchezo huo klabu ya Sutton United ilipewa alama 8-1 katika kampuni za ubashiri wa matokeo hivyo kwa kila aliyebashiri matokeo ya mchezo huo na kuipa ushindi Sutton United, kiwango cha fedha ambacho angeweka kingezidishwa mara nane.


Siku ya mchezo husika Wayne Shaw alionekana kuwa ni mtu mwenye pilika pilika za hali ya juu kwani kabla ya mchezo dhidi ya Arsenal alionekana akikata majani, wakati wa mapumziko alionekana akiwa Bar, katika kipindi cha pili alionekana akila pizza.

Hata hivyo vitko vyake viliendelea tena asubuhi kwani muda mchache kabla ya kujiuzulu alionekana katika mahojiano na kipindi cha Goodmorning Britain, kabla ya kukamatwa na polisi kwaajili ya kesi ya kubeti wakati yeye ni mchezaji majira ya saa saba mchana (13:00).


Ilipofika saa tisa na dakika arobaini na tano (15:45) akatangaza kustaafu kucheza soka.

0 comments:

Post a Comment