Posted by Williammalecela.com on Wednesday, February 08, 2017
Taarifa ilimfikia kila Mtanzania kuwa rapa kutoka A- Town LORD EYES, amesainiwa na lebo mpya ya muziki 'BANA' inayomilikiwa na Mwimbaji wa Bongo Fleva Barakah The Prince.
Lord Eyes bado anatajwa kama Memba wa kundi la WEUSI.. Je Weusi wanasemaje??? Kupitia 255 ya XXL Clouds FM leo, Msemaji wa kundi la Weusi NIKKI WA PILI ametoa ufafanuzi kuhusu kusainiwa kwa Lord,
"Ahh mimi pia nasikia stori hizo kama zinavyo sikika kwenye media, mbali na hapo sijui ukweli wake wala uhalisia wake ukoje, labda Lord Eyes mwenyewe anaweza kuitolea maelezo zaidi."- alisema Rapa Nikki Wa Pili.
Kukazia stori hii, @NikkwaPili alisema hawajawahi kuzungumza na rapa huyo juu ya ishu hii.
0 comments:
Post a Comment