Friday, February 3, 2017

Umeisikiliza  vizuri ngoma ya “Sinaga Swagga” yakwake Young Killer? Kama jibu ni ndio naamini utakuwa unalitambua hili la kuwepo na mistari ya diss kwa rapper Young Dee ndani ya ngoma hiyo.

Unachotakiwa kukifahamu ni kwamba tangu ngoma hiyo imetoka rapper Young Killer pamoja na Young Dee walikuwa hawajawahi kukutana face to face,  sasa juzi kama Mungu tu, wawili hao wakakumbana studio kwa Mr T-Touch pande za Sinza Dar es Salaam.
Unaambiwa kidogo wachapane mikono humo ndani bahati nzuri Legendary Dully Sykes alikuwepo na kutumia ukubwa na hekima zake kuwatuliza madogo hao.
Ubuyu kamili ameumwaga Soudy Brown leo kwenye U-Heard ya XXL, na kama ilivyo kaida nimeukusanya na kukuwekea hapa chini kwenye video hii ili na wewe uweze kuumung’unya kiulaini.
Play hii video hapa chini kumsikia Soudy brown akipiga story na wote wawili baada ya tukio hilo kutokea na umsikilize kila mmmoja anavyojitapa mbele ya mwenzie.

0 comments:

Post a Comment