Thursday, February 9, 2017



Aliekuwa bingwa wa dunia mara 14 katika mchezo wa gofu, Tiger Woods amesema kwa sasa hana furaha tena kwani majeruhi ya mara kwa mara yanayomkabili yanamfanya ashinwdwe kurudia enzi zake za kung’ara katika mchezo huo.


Woods, 41, ameyasema hayo ikiwa ni siku chache toka alipolazimika kujitoa katika michuano ya jangwani huko Dubai, Dubai Desert Classic katika hatua ya pili ya michuano hiyo kutokana na maumivu ya mgongo.

Hili ni pigo kubwa kwa Tiger Woods kwani alirejea uwanjani mwezi December akitokea kuuguza majeraha ya muda mrefu.


Tiger Woods amesema mara baada ya kukaa nje ya mchezo wa gofu kwa miezi 15 aliamini kwamba angerejea rasmi katika mchezo huo na kupambana ili kurejesha heshima aliyokuwa amejizolea siku za nyuma.

Kutoka mwaka 2015 hadi sasa Tiger Woods hajafanikiwa kutwaa taji lolote na katika michuano kadhaa aliyoshiriki amekwa akipata matokeo mabaya.

Katika michuano ya Hero World iliyoshirikisha wachezaji 18 wa mchezo wa gofu, Tiger woods alimaliza katika nafasi ya 15 kati ya watu 18 kwenye michuano ambayo ilifanyika huko Bahamas.

0 comments:

Post a Comment