Kuna wakati unatamani kujua watu wanawaza nini juu yako. Kupitia kipindi namba moja cha maswali na majibu cha Papo kwa Papo na Papi kinachofanyika kila siku ya Jumatano kwa kutoa platform ya watumiaji wa mtandao wa Twitter kuuliza maswali kwa mgeni atakaye alikwa kwenye kipindi hicho.
Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba aliwekwa mtu kati na haya ni zaidi ya maswali 70 aliyoulizwa;
Mtoto wa vitoto Eido @MtotowaVitoto
@papokwapapoTZ #AskRuge Urafiki wake na Joseph kusaga Ulianzia wapi hadi wakaaminiana kiasi kikubwa hivi Kwenye Biashara????
Hakuna Matata

@MGoyayi
Ruge ni muajiriwa au ni mmoja wa wamiliki wa Clouds Media group? #AskRuge @papokwapapoTZ
iKarata @Karatajr_
#AskRuge Ni kitu gani unahisi Joseph Kusaga anaweza kufanya wewe huwezi na ungetamani siku moja uweze kukifanya?? @papokwapapoTZ
Cherie tigress @TigressCherie
Ikitokea mtu akapanda dau la kukuhamisha clouds media group unaweza hama sababu ya maslahi??@papokwapapoTZ #AskRuge
Pappy @boipapy
Redio clouds na chama tawala CCM vina uhusiano gani wa kibiashara na kisiasa? #AskRuge
Sir @chedy_Wang
Kuna Skendo Iliyokunyima Raha Ukatamani Kuacha Kuwa Boss Wa Clouds ..? #AskRuge
DJ spata

@official_spata
nyie kama clouds mkitaka kuajili mtu yeyote mnaangalia vigezo vipi ?? #AskRuge
@Ucrah
Inasemekana wewe/kampuni yenu ndiyo chanzo cha kutokuwepo kwa maelewano kati ya Lady Jaydee na MwanaFA, unasemaje kuhusu hili? Na je, kama si kweli, una mpango upi juu ya kuwapatanisha wasanii hawa?
Agustino Reginald @AgustinoJr
Kwann watu wengi wana fikra kuwa Unawanyonya Wasanii wako Kutoka Tht #AskRuge
EDEN-10+ @MarcEden4
Kwanini kila msanii wa kike akienda pale T. H. T unamtaka kimapenzi ili tu aweze kutoka ki,music?? #AskRuge
PYT @IvonneNanyaro 4h4 hours ago
Nini kimetokea baina yako na msanii Ruby? #AskRuge #PapoKwaPapoNaPapi
Jessica @JessicaSanga
Wasanii kama Ally Nipishe, Beka, Pipi, Amini, Ditto hawajafika mbali tatizo ni nini hasa?#AskRuge @papokwapapoTZ
juma mzuzuri @jiham08
Mliishia wapi katika biashara ya mitindo mliotaka kuanzisha pale THT na je hao watu walienda China mafunzoni @papokwapapoTZ #AskRuge
Pappy @boipapy
Je wewe na majizzo ni washkaji? #AskRuge
Baba Adyan @DeoMruah
Je huwa unasikiliza E-FM? #AskRuge
Shamim Omar @MimurOmar
Ujio wa Efm ushidani na upokonyaji wa watangazaji, hasara na faida gani mumeipata? #AskRuge @papokwapapoTZ
alpha abdalah wawa @alpha_abdalah
Unamshauri nini majizo ili @Efm937 ikue kama @CloudsMediaLive #AskRuge
Dante @DanteThePrince
Unazungumziaje adhabu ya TCRA kwa kipindi cha Take One. Imewaathiri vipi? #AskRuge
Lucas_tz @LucasKifyasi
#AskRuge @papokwapapoTZ Tunashuhudia baadhi ya watangazaji wakichochea bifu za wasanii je hii ndio strategy yenu ya kuwafikia wasiklizaj?
Uncle sAm @Ankal_Sam
Baadhi ya wasanii Ulaya na Marekani wametumia Bifu zao kupiga hela, unazungumziaje bifu za wasanii wa kibongo?? #AskRuge #PapoKwaPapoNaPapi
JK @JaffaryKaloka
#AskRuge Ushindani kati ya Diamond na Alikiba uendelee? Na je una tija kwa wao binafsi na mziki wa Tanzania kwa ujumla? @papokwapapoTZ
MFALME @CndaKing
Hiki kibeef cha wanamiziki wetu wanaoimba kama fursa hivi? Sijui kama umefikiria mwisho wa siku kitengeneze pesa pale taifa? #AskRuge
JohLen @John_MushL
Unazungumzia vipi issue ya wafanyakazi wako kutoka na kurejea mjengoni+work performance yao (from clouds to efm)#AskRuge #PapoKwaPapoNaPapi
zlatan @GGodrigo
Tumefanikiwa kumrudisha Paul James na Gadner Mjengoni Vipi kuhusu Dina Marious? #AskRuge
BlackVirus @allen_mike1
#AskRuge kwanini mlibadlisha jina la tamasha kutoka summer-jam na kuwa Fiesta?
Stambuli @junior_becca
Tumeona mmefanya vizuri ktk matamasha makubwa (FIESTA). Ukiwa kama mkurugenzi umeshawahi kufikiri kuhusa suala TUZO kwa wasanii? #AskRuge
Ahmed Asas @ahmedsalimasas
Hivi ilikuaje mkoa wa Iringa iliondolewa kwenye Ratiba ya Fiesta. @papokwapapoTZ #AskRuge
Abduli @Abdulswahib_
Msanii Wa Nyumbani Analipwa Kiasi Gani Kwenye Show Moja Ya Fiesta? (Kiwango Cha Chini Kabisa) @papokwapapoTZ #AskRuge
Christopher @ChrisMkapa
Ni kweli Kuna uhusiano wa kimaslahi Kati ya clouds na ccm? #AskRuge @papokwapapoTZ
Gäbbÿ @majaliwagab
@papokwapapoTZ clouds media Group wanampango wa kuanzisha Awards kama za BET? #AskRuge
ray @rOmSoi
#AskRuge Ni Kwa Kiasi Gani Semina Za Fursa Mlizotoa Zimewasaidia Watu Kuchangamkia Fursa Zilizopo Hapa Nchini? Cc @papokwapapoTZ
KIJANI the DREAM @simbahd
Je mmekuwa mkifanya tathmini ya matokeo ya seminar za fursa? je performance ikoje na nani ni mfano hasa wa fursa tangu ianze? #AskRUge
L I U @d33dat
Umekuwa Inspirational sana kwenye dhana ya ujasiliamali na fursa za kilimo, Je? wewe binafsi unashughulika na kilimo? #AskRuge
Scooby Askari Wa

@incredible_nory
Kwa kifupi tu;nisikupotezee muda Mkuu… Unaeza ukatuelezea kwa machache sakata lako na T.I.D lilivyokua?! #AskRuge
ustine Bisangwa @jwise017
Nini kiliipata Smooth Vibes? #AskRuge
saeed tutla @tutla7
mwaka moja wa @MagufuliJP una uzungumziaje na tutegemee nin mbeleni #AskRuge @papokwapapoTZ
Mahmud @MahmudKullane
Tumesikia Rais akiisifia CloudsFM, ungekuwa mkurugenzi wa TBC ungejisikiaje Rais anaisifia radio binafsi badala ya idhaa ya Taifa #AskRuge
BeingAidanCharlie @AidanCharlie
Top 5 ya watangazaji wako bora wa kizazi cha sasa #AskRuge
ViCtOr @mwangathegreat
Una ushauri gan kuhusu soko la mziki hasa ktk upande wa album kufa na vp khs blogs kuweka nyimbo za wasanii bure #AskRuge @papokwapapoTZ
Charlie Bihemo™ @Charliebihemo
Kitu kimekosekana kwenye mziki ambacho unashauri kiwepo ili kufanya mziki wetu ufike mbali zaidi @PapiChulo_Chuly @papokwapapoTZ #AskRuge
Mussah @somebarry
Ni wazi ujio wa mitandao ya kijamii umeua ‘nguvu’ ya cloudsfm maana zamani msanii usipopigwa clouds hutoboi. Haikuumizi kichwa? #AskRuge

roujer

@Officialchico8
Ugomvi wako na sugu uliisha vp #AskRuge @papokwapapoTZ @PapiChulo_Chuly
Hakuna Matata

@MGoyayi
Kuna wakati nilisikia Clouds wameanzisha kituo cha kimataifa Dubai. Kimefikia wapi? #AskRuge #PapoKwaPapoNaPapi
dennis @denisurio
Maamuzi ya clouds yanafanywa na management au wewe, kwanini ukitofautiana na mtu nyimbo zake hazipigwi clouds. #AskRuge

roujer

@Officialchico8
Nini kilitokea kwa dina marios mpka akaondoka clouds mana tuliambiwa anapewa kipindi cha tv @papokwapapoTZ @PapiChulo_Chuly #AskRuge
JK @JaffaryKaloka
#AskRuge Ni kweli mziki wa Hiphop ni mgumu kibiashara ukilinganisha na mziki wa kuimba? @papokwapapoTZ
Salum Ahmed @54LUM
Ulivyokuwa na beef na Sugu uliwah kuskiliza zile diss tracks walizokuwa wanaiponda kampuni yako?? #AskRuge @papokwapapoTZ
Khatibinho Jr @OfficialKhatib
Harakati za AntiVirus zilikusumbua kama ulivyosema, umejifunza nini kupitia zile harakati? #AskRuge @papokwapapoTZ @PapiChulo_Chuly
Simba Wa Kuchora @1960Remija
#AskRuge unaiona wapi Clouds Media ndani ya miaka 5 ijayo? JPM alipoomba mualiko wa Fiesta, mlimualika au mlipotezea? #PapoKwaPapoNaPapi
Aymanny

@Addy_Adams
Vp ule utaratibu wa kuwalipa Wasanii kwa nyimbo zinapochezwa unawezekana kwa Tz? Na km hauwezekani ni kwann labda? #AskRuge @papokwapapoTZ
♛ EugyzLulu

@Messizlulu
Unachukuliaje ile ishu ya Lady JD. Je kuna mpango wa kutatua na kuyajenga? #AskRuge
Sosiholics @sosiholics
Take one kilifungiwa nadhani n kwa sababu ya kufanya mahojiano na yule shoga je we unadhani serikali IPO sawa? Na kama ndio Y? #AskRuge
Ngaranian Hangaza @YakoSio
Tulisikia upande wao lakini wewe na Kusaga hamjawahi kuzungumzia hili. Nini hasa kilisababisha Masoud na Fina wakaondoka Clouds? #AskRuge
Kivuruge @salim_alkhasas
Kwenye XXL ulisema hujui uanzie wapi, tunaomba uanzie popote pale, nini mbaya ishu ya TID mnyama? #AskRuge
Sosiholics @sosiholics
#AskRuge Kwa habari ambazo hazijadhibitishwa/sina uhakika nazo eti nasikia Yamoto bendi wameanza kupotezewa na clouds kwa sababu wanakudai
Jamaa @Ngalawajr
Unapata nafasi kumshauri Mh.Rais kuhusu sera zake za uchumi,Upi utakuwa ushauri wako bora kabisa? #AskRuge
Ebrahim Issally @eissally
What is your biggest fear #AskRuge @papokwapapoTZ
король @kiddiography
Taja fursa 5 kwa kijana asie na kipato (au mtaji kidogo) kwenye uchumi wa Tz kwasasa. #AskRuge
Yakivil Jumalism @yakiviljumalism
Kwa mujibu wa tafiti #TBC1 imekuwa ya mwisho kutazamwa,unafikiri tatizo ni nini kwa chombo chetu cha taifa? #AskRuge @papokwapapoTZ
Calvin @KelvinMwaipungu
#AskRuge Kwanini @CloudsMediaLive inatumika na viongozi wengi wa kiserikali kutoa matamko yao kuliko TBC? mfano Makonda .. @PapiChulo_Chuly
Sebastian @sebamwasele
Mmeshiriki kikamilifu katika ziara ya Mkuu wa Mkoa mafanikio yenu ni yapi Je mna mpango wa kushiriki ziara za wakuu wengine?#AskRuge
The Pearl @WalleLulu
Mmeandaa nini kwa vijana walijitolea kusapoti brand yenu maana kuna hata magrup ya WhatsApp kwa ajiri ya kusapoti clouds #AskRuge
EDEN-10+ @MarcEden4
Kwanni mnawapangia wasanii aina ya music kuimba ili wapate kupgiwa nyimbo zao kwenye radio yako? #AskRuge
Abdallah® @SamataJr_12
#AskRuge kwanini haupigi nyimbo za @RamaDee3 radioni kwenu @cloudsfm hizo taratibu zinazozuia kupigwa kwa nyimbo zake ni zip? Tuweke wazi
Ahmed Asas @ahmedsalimasas
1/2 Gharama za kutangaza matangazo Clouds ni kubwa kulingana na Vituo vingine. mmejipanga vipi kuwakamata hata wale ambao sio makampuni makubwa kuja kuleta matangazo kwenu?
#AskRuge
Mtickasön Unchained @mtickz
Hivi Fiesta kuleta wasanii wa mbele ndo basi tena au sio? #AskRuge @papokwapapoTZ
The Man Himself

@Elycaptano
Tuambie mahusiano yako na P-Funk wa Bongo Records yako vipi?? #AskRuge
#AskRuge Unamzungumziaje marehemu Amina Chifupa? na nilini mara ya mwisho umemtembelea mtoto wa marehemu?#PapoKwaPapoNaPapi @papokwapapoTZ
Uncle Fafi @Tanganyikan
Hivi karibuni Clouds imekuwa kinara wa kupiga nyimbo za Naija.. huoni mnachangia kubomoa nyumba mliyotumia nguvu kuijenga? #AskRuge
shamim mwasha @8020FASHIONS
#AskRuge Inakuwaje kila msanii /mtangazaji wa kike wanaotaka kutoka watoe hongo ya ngono kwako ? #PapoKwaPapoNaPapi
zlatan @GGodrigo
Vipi mzee Ruge ushawahi kupima ukimwi? #AskRuge
pedro shette @boshette
#AskRuge kilio changu choice fm, mliamua kui’re-vamp’ ikapoteza ladha tuliyoipendea. sababu ya kuibadilisha ni ipi? #PapoKwaPapoNaPapi
DadaYule @kubwazawadada
Wasanii wa kike bado wapo nyuma sana kimuziki bado hawajafikia kasi ya ali na dai nyie kama media mna mkakati gani wa kuwainua #AskRuge
Kiduo.M.Mgunga @mgungakiduo
Unajivunia kufanya kazi Clouds Media ?.Utakumbukwa kwa lipi ukitoka Clouds Media ?.@papokwapapoTZ #AskRuge
Natasha @TasherP
Ni Nani unafikiri anaweza chukua nafasi yako ya kazi akaimudu vizuri na kuziba uwepo wako?? #AskRuge @papokwapapoTZ
Source kwa hisani ya #PapoKwaPapoNaPapi
0 comments:
Post a Comment