Aliyekuwa mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan ameripoti polisi leo asubuhi baada ya kuambiwa afanye hivyo.
Azzan amesema tangu watu waanze kumzungumzia kuhusiana na dawa za kulevya ni muda mrefu na hivyo amezungukwa na maadui wengi.
"Mimi tangu nianze kuzungumzwa sijaanza leo, wanasikiliza kwenye mitandao ya kijamii, hawajui mimi nina maadui wangapi ambao wananizunguka. Utakuta mtu tu ananitaja kwa chuki zake," amesema Azzan.
Wakati huo huo, Mchungaji Josephat Gwajima aliyedai angekwenda kuwaona wenzake waliosalia polisi, naye pia ameripoti polisi saa 10.46 asubuhi
Msaidizi wa askofu huyo amesema Gwajima ametakiwa kuripoti tena mchana huu.

0 comments:
Post a Comment