Monday, February 6, 2017


Baada ya watu wengi kudai kwamba tukio la wizi alilofanyiwa Nicki Minaj nyumbani kwake limesababishwa na Meek Mill, Meek ameamua kufunguka na kusema yeye hausiki juu ya ishu hiyo.

Hivi karibuni wakati Nicki Minaj akiwa anasherehekea muungano wao wa Young Money, kuna sakata jingine baya lilitokea nyumbani kwake kwa kuibiwa vito vya thamani, Sasa baada ya ishu hiyo mashabiki wengi wakaanza kufunguka juu Meek Mill kwamba yeye atakuwa amehusika kutokana na jinsi walivyoachana na Nicki.
Kupitia mahojiano ambayo mtandao wa Tmz ulifanya na Meek Mill, katika klabu ya life huko Huston Texas, Meek alifunguka kwa kusema kwamba “Naonekana kama nawaibia watu?, nina $450k kwenye shingo yangu, $80k mkono wangu, bado naonekana kama nawaibia watu.

0 comments:

Post a Comment